RONALDO APIGA ZOTE MBILI REAL IKING'ARA LA LIGA, BALE HAKUWEPO KABISAAA
PAMOJA na kumkosa mchezaji ghali duniani, Gareth Bale,
lakini mchezaji anayeliwa mshahara mkubwa zaidi duniani, Cristiano Ronaldo
alitosha kuipa pointi tatu Real Madrid usiku huu, baada ya kufunga mabao yote
katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Elche.
Bale atarejea katika mechi ya nyumbani na Atletico Madrid
Jumamosi wakati leo Ronaldo, ameendelea kuiweka Real karibu vinara wa La Liga.
Ronaldo alifunga mabnao hayo katika dakika za 51 na dakika
ya sita ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90, wakati bao la kufutia
machozi la Elche lilifungwa na Richmond Boakye dakika ya pili ya muda wa
nyongeza baada ya kutimua dakika 90.
Kikosi cha Elche kilikuwa: Elche: Manu Herrera; Damián,
Botía, Lombán, Albácar; Rubén Pérez, Carlos Sánchez; Stevanovic, Coro, Fidel na
Boakye.
Real Madrid: Diego López, Pepe, Ramos, Coentrão, Khedira,
Ronaldo, Benzema, Arbeloa, Modric, Di María na Isco.
Raha: Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Madrid bao la
pili
Moja zaidi: Cristiano Ronaldo akishangilia na wachezaji
wenzake
Weka kule: Real Madrid ilicheza bila mchezaji ghali duniani,
Gareth Bale
Beki wa Elche, Botia (kushoto) akikabiliana na mshambuliaji
Mfaransa wa Real Madrid, Karim Benzema
















.jpg)








0 comments:
Post a Comment