AKINA SAMATTA, ULIMWENGU WAANZIA UGENINI NUSU FAINALI AFRIKA NA MAZEMBE YAO
TOUT Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC), itaanzia ugenini Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika
dhidi ya Stade Malien ya Mali, Oktoba 6, mwaka huu, kabla ya kurudiana wiki
mbili baadaye mjini Lubumbashi.
Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka
Afrika (CAF) jana, mchezo wa kwanza utachezwa kwenye Uwanja wa Modibo Keita
mjini Bamako kuanzia saa 10:00 jioni kwa saa za huko na saa 12:00 kwa saa za
Afrika Mashariki.
Mapacha watatu; Kutoka kulia Thomas Ulimwengu, Tresor Mputu
na Mbwana Samatta washambuliaji hatari wa Mazembe ambao wanafunga karibu kila
mechi
Mechi hiyo itachezeshwa na refa Alioum Neant, atakayesaidiwa
na Evarist Menkouande wote wa Cameroon na Peter Edibi wa Nigeria, wakati refa
wa akiba atakuwa Mohamadou Mal Souley pia wa Cameroon.
Timu hizo zitarudiana Oktoba 19, Uwanja wa Mazembe mjini
Lubumbashi, zikichezeshwa na marefa Haimoudi Djamel wa Algeria atakayesaidiwa
na Achik Redouane wa Morocco na Etchiali Abdelhak wa Algeria, wakati refa wa
akiba atakuwa Bousseter Sofiane wa
Algeria pia.
Mazembe inayoongozwa na washambuliaji wawili wa Kitanzania,
Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu, ikifanikiwa kuitoa Stade
Malien itamenyana na mshindi wa Nusu nyingine, kati ya timu za Tunisia tupu,
Club Africaine na C.S. Sfaxien.
Ikumbukwe Mazembe iliangukia kwenye Kombe la Shirikisho
baada ya kutolewa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika 16 Bora ya Ligi ya
Mabingwa Afrika msimu huu na sasa inaelekea kufuta machungu kwa kutwaa taji
hilo la pili kwa ukubwa kwa michuano ya klabu Afrika.













.jpg)








0 comments:
Post a Comment