MANJI AWATULIZA WACHEZAJI YANGA SC, AWAAMBIA HANA NOMA NAO, AMVUTA NGASSA PEMBENI WAYAMALIZA 'KIKUBWA'
MWENYEKITI wa Yanga SC, Alhaj Yussuf Mehboob Manji
amewaambia wachezaji wa timu hiyo kwamba hana matatizo nao kwa matokeo ya awali
ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na amewataka waelekeze nguvu zao katika
mechi zijazo.
Yanga imeambulia pointi sita katika mechi tano za awali za
Ligi Kuu ya Vodacom, kutokana na sare tatu, kushinda moja na kufungwa moja,
hivyo kuachwa kwa pointi tano kileleni na wapinzani wao wa jadi, Simba SC.
Jana Manji alikutana kwa chakula cha jioni na wachezaji wa
timu hiyo katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam akiwa ameambatana na Makamu
wake Mwenyekiti, Clement Sanga, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Isaac Chanji na
Mjumbe wa Sekretarieti, Patrick Naggi.
Manji akipeana mkono na Chuji alipokutana na wachezaji hao
mwaka jana.
Katika kikao hicho, Manji aliwaambia wachezaji wa Yanga
hamlaumu yeyote kwa matokeo hayo, kwani ligi bado mbichi, ila akawataka
waunganishe nguvu zao kuelekea mechi zijazo, ili kurejesha ushindi na furaha
klabuni.
Pamoja na hilo, Manji alizungumzia suala la madai ya baadhi
ya wachezaji ya fedha za usajili na akaliweka sawa kwa wale ambao walikuwa
wanadai kuwawekea utaratibu wa malipo haraka, jambo ambalo Naggi ametakiwa
kuhakikisha analishughulikia mara moja.
Aidha, Manji baada ya kikao cha pamoja na wachezaji wote, alimvuta
pembeni Mrisho Ngassa kujadiliana naye faragha.
Haikujulikana mara moja Manji alizungumza nini na Ngassa,
lakini inaweza kuwa kuhusu deni analotakiwa kuilipa Simba SC, Sh. Milioni 45
kwa kosa la kusaini Mikataba na timu mbili. Ngassa alifungiwa mechi sita za
mashindano na kutakiwa kurejesha fedha alizochukua Simba SC Sh. Milioni 30
pamoja na fidia ya Sh Milioni 15.












.jpg)








0 comments:
Post a Comment