MAN UNITED YAICHAPA LIVERPOOL 1-0 KOMBE LA LIGI
MACHO yote yalikuwa kwa Luis Suarez baada ya kurejea
Liverpool kufuatia kumaliza adhabu yake ya mechi 10, lakini Javier Hernandez akaiteka
shoo kwa bao lake pekee lililoipeleka Manchester United Raundi ya Nne ya Kombe
la Ligi, maarufu kama Capital One.
Hatimaye Suarez alicheza mechi yake ya kwanza ya msimu mpya
baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake ya kumng'ata beki wa Chelsea, Branislav
Ivanovic msimu uliopita.
Na wakati mshambuliaji huyo wa Uruguay alizomewa na
mashabiki Uwanja wa Old Trafford, alikuwa ni Chicharito aliyepoza maumivu ya
David Moyes kufuatia kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa wapinzani, Manchester City
katika Ligi Kuu Jumapili.
Liverpool ilitawa sehemu kubwa ya mchezo na Daniel Sturridge
alipoteza nafasi kadhaa nzu za kufunga, lakini Hernandez hakufanya makosa
alipopata nafasi dakika ya 46.
Wayne Rooney, ambaye ndiye mchezaji bora zaidi kwa United
hivi sasa, alipiga kona nzuri baada ya mapumziko na Hernandez akaunganisha
nyavuni.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Rafael Da
Silva, Smalling, Evans, Buttner, Jones, Giggs, Nani, Rooney, Kagawa na
Hernandez.
Liverpool: Mignolet, Toure, Skrtel, Sakho, Jose Enrique,
Gerrard, Lucas, Henderson, Suarez na Moses, Sturridge.
Shujaa: Javier Hernandez akishangilia baada ya kufunga bao
pekee la Manchester United Uwanja wa Old Trafford













.jpg)








0 comments:
Post a Comment