RHINO RANGERS YAISHUSHA YANGA LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA ASHANTI UNITED LEO TABORA
RHINO Rangers imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara msimu huu, baada ya leo kuilaza Ashanti United mabao 2-0
Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora.
Kwa ushindi huo, timu hiyo ya Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) imefikisha pointi saba na kupanda hadi nafasi ya nane ikiwashusha kwa
nafasi moja, mabingwa watetezi, Yanga SC.
Juu ya mabingwa; Rhino leo wameishusha Yanga kwa nafasi moja
Katika mchezo huo, mabao ya Rhino yalifungwa na Kamana Salum
dakika ya 26 na Hussein Abdallah dakika ya 64.
Ligi hiyo itaendelea Jumamosi wakati, Yanga SC
itakapomenyana na Ruvu Shootings Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Rhino
Rangers wakiikaribisha Ashanti United Mwinyi, Tabora.
Mechi nyingine zitapigwa Jumapili, Simba SC ikishuka dimbani
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na JKT Ruvu, Rhino Rangers na Kagera
Sugar Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora, Mbeya City na Coastal Union
Sokoine, Mbeya, Mgambo JKT na JKT Oljoro Mkwakwani, Tanga na Ashanti United na
Mtibwa Sugar, Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.













.jpg)








0 comments:
Post a Comment