NGASSA AGOMA KUSAINI HATI YA YANGA SC KUMLIPIA DENI LA SIMBA SC, APATA BONGE LA OFA UARABUNI
MRISHO Khalfan Ngassa amepata timu ya Oman inayotaka
kumnunua kutoka Yanga SC pamoja na kulipa deni la Simba SC, Sh. Milioni 45,
lakini uongozi wa klabu yake kama unamuwekea kauzibe hivi.
Habari za ndani ambazo BIN ZUBEIRY imezipata juu ya sakata
la Ngassa na Yanga ni kwamba, mchezaji huyo amepata timu inayotaka kumnunua
moja kwa moja, ikiwa tayari kutoa kiasi cha Sh. Milioni 100, ambazo zitalipa
deni la Simba na nyingine kulipwa Yanga ambao wana Mkataba naye kwa sasa.
Hata hivyo, wakati Yanga ikimzuia Ngassa kwenda Oman, nayo
inaonekana kusuasua kumilipia deni la Simba SC.
Habari zinasema Yanga wametaka kumsainisha Ngassa Mkataba wa
kumlipia deni, lakini amegoma kuusaini kwa kuhofia kurudia kosa alilofanya
kusaini Mkataba na Simba SC ambao hakuuelewa.
Mpenzi wa Yanga; Mrisho Ngassa amegoma kusaini kichwakichwa
fomu za kulipiwa deni
“Ngassa ameshituka sasa hivi, amegoma kusaini huo Mkataba wa
kulipiwa deni, kwanza hadi aupeleke kwa Wakili wake akaupitie. Unajua Simba
walimuambia anasaini kukubali kucheza kwa mkopo, kumbe anasaini Mkataba mpya,
sasa amekuwa mjanja sana sasa hivi,”kilisema chanzo.
Chanzo hicho kimesema kwamba, Yanga inataka kumlipia Ngassa
deni na kuongeza miaka miwili katika Mkataba wake kutoka miwili ya sasa, lakini
yeye mwenyewe mchezaji amependekeza alipiwe deni hilo na baada ya hapo atakuwa
anakatwa kwenye mshahara wake.
Hadi sasa Ngassa hajasaini hati aliyotakiwa kusaini alipiwe
deni hilo, maana yake kuna hatari akashindwa kuanza kucheza Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ikumbukwe Ngassa alifungiwa mechi sita za mashindano kwa
kosa la kusaini Mikataba na timu mbili, Simba na Yanga SC. Pamoja na adhabu
hiyo aliyomalizia Jumapili, Ngassa alitakiwa kurejesha fedha alizochukua Simba
SC Sh. Milioni 30 pamoja na fidia ya Sh Milioni 15, jumla Milioni 45.













.jpg)








0 comments:
Post a Comment