MAMLAKA MWANZA ZAAHIDI NYASI BANDIA NYAMAGANA
MAMLAKA za Mkoa wa Mwanza zimesema zitatimiza ahadi yao ya kuchangia
dola 118,000 za Marekani (zaidi ya sh. milioni 190) ili kukamilisha mradi wa
kuweka nyasi bandia kwenye Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza kabla ya Oktoba
15 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja
na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula wametoa ahadi hiyo wakati
wa kikao kati yao na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Leodegar Tenga kilichofanyika leo (Septemba 25 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga (wa pili kushoto) akiwa na
ujumbe wa Mkoa wa Mwanza ulioongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mhandisi Evarist Ndikilo
ulipomtembelea katika ofisi za TFF jana. Wa tatu kutoka kushoto ni Mstahiki
Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula akifuatiwa na Mkurugenzi wa Jiji la
Mwanza, Hida Hassan.
Wakuu hao wa Mwanza katika kikao hicho pia walifuatana na
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Hida Hassan.
TFF ilipeleka mradi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) wa Goal Project IV wa nyasi bandia wa dola 500,000 za Marekani
katika Uwanja wa Nyamagana.
Mradi huo ulipelekwa huko baada ya Mkoa wa Mwanza kuahidi
kuchangia dola 118,000 ili kukamilisha thamani ya mradi mzima ambayo ni dola
618,000 za Marekani. Wamiliki wa uwanja huo ni Jiji la Mwanza.
Goal Project I ilitumika kwa ajili ya ujenzi wa hosteli ya
TFF (technical centre), Goal Project II nyasi bandia Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume wakati Goal Project III iliweka nyasi bandia katika Uwanja wa Gombani
ulioko Pemba, Zanzibar.













.jpg)








0 comments:
Post a Comment