KLABU ya Arsenal itamenyana na wapinzani wao katika Jiji la
London, Chelsea katika Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One
Cup baada ya kuitoa West Brom kwa penalti 4-3 Uwanja wa Hawthorns.
Mechi hiyo imeisha kwa sare ya 1-1 usiku huu, lakini penalti
walizokosa Morgan Amalfitano na Craig Dawson zinawasongesha mbele Gunners.
Mbele: United imesonga mbele kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya
Liverpool Uwanja wa Old Trafford
RATIBA KAMILI RAUNDI YA NNE CAPITAL ONE
Sunderland v Southampton
Leicester City v Fulham
Birmingham City v Stoke City
Manchester United v Norwich City
Burnley v West Ham United
Arsenal v Chelsea
Tottenham v Hull City
Newcastle v Manchester City
Mechi zote zitachezwa Jumanne ya Oktoba 29 na Jumatano ya
Oktoba 30.
Manchester United baada ya kuwatoa wapinzan wao, Liverpool
watamenyana na Norwich nyumbani katika Raundi ya Nne.
Bao pekee la Javier Hernandez mapema kipindi cha pili katika
ushindi wa 1-0 Old Trafford, linawakutanisha Mashetani Wekundu na The Canaries
Oktoba 28.
Birmingham iliyowatoa mabingwa watetezi Swansea kwa mabao
3-1 watacheza tena nyumbani katika 16 Bora, safari hii wakimenyana na timu ya
Mark Hughes, Stoke.
Licha ya kupangiwa wapinzani wagumu, lakini The Blues bado
wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa tena taji walilolitwaa mwaka 2011, na United
ikiwa timu nyingine inayopewa nafasi pia baada ya kupangiwa Norwich.
Katika mechi nyingine, Newcastle itaikaribisha Manchester
City Uwanja wa St James Park baada ya kuwatoa Leeds, wakati Hull wataifuata
Tottenham siku kadhaa baada ya kucheza mechi ya Ligi Kuu, Uwanja wa White Hart
Lane.
Timu isiyo na kocha kwa sasa, Sunderland itamenyana na
Southampton, wakati West Ham watakwedna Kaskazini kumenyana na Burnley.
Fulham ya Martin Jol itaifuata Leicester kusaka nafasi ya
Robo Fainali.
MIKWAJU YA PENALTI
West Brom: Reid (penalti ya kwanza) amefunga, Rosenberg
amefunga, Morrison amefunga, Dawson amekosa, Amalfitano amekosa
Arsenal: Bendtner amefunga, Gnabry amekosa, Olsson amefunga,
Akpom amefunga, Monreal amefunga
Arsenal imeifunga West Brom kwa penalti 4-3
Arsenal iliendeleza wimbi la ushindi kwa kuitoa kwa matuta
West Brom Uwanja wa The Hawthorns na kuingia Raundi ya Nne.
Eisfeld aliifungia Arsenal dakika ya 61 kabla ya Berahino
kusawazisha dakika ya 71.
Kikosi cha West Brom kilikuwa: Daniels, Reid, Popov, Lugano,
Dawson, Sinclair, Dorrans, Mulumbu/Morrison dk91, Berahino/Amalfitano dk101,
Long/Rosenberg dk91, Sessegnon
Arsenal: Fabianski, Mertesacker, Vermaelen, Monreal,
Jenkinson, Arteta/Bellerin dk95, Miyaichi, Gnabry, Hayden/Kris Olsson dk84,
Bendtner, Eisfeld/Akpom dk82.
Ya ushindi: Nacho Monreal akiifungia Arsenal penalti ya
ushindi
0 comments:
Post a Comment